Thursday, January 12, 2017

Dondoo za Ukulima wa Miti. #Smartyforestry

Take a look at @pelezi's Tweet: https://twitter.com/pelezi/status/819467612111458304?s=09

Wednesday, November 13, 2013

"Mazingira yatutunze" Environment day-2011, Tangeni,Morogoro.

Pupils singing Mazingira song "Mazingira yatutunze" that was the message in
this song in the Environment day-2011, Tangeni, Mvomero district, Morogoro.
Youth are incouraged to conserve their environments through environmental education.

Friday, November 8, 2013

The Botanist - Mr. C.K. Ruffo


Conducted many Botanical surveys and forest inventories in Tanzania.

Collected over 5,000 botanical specimens in Tanzania, Kenya and United Kingdom

Sanrafaeria ruffonammari Verdc. A new plant from East Usambara was honoured to him by Bernard Verdcourt of Royal Botanic Gardens, Kew, England in 1998. The specimen was Ruffo & Mmari 1739 (K, holotype; TFD, isotype). Collected from Kwamgumi Forest Reserve, Muheza District, Tanga, Tanzania. Floristic Region T3, in November, 1986.

Identification and labelling of plants at the State House in Dar-es-salaam in 1971 and 1977 and Zanzibar State House in 1981.

 Resurveying and labelling of plant species in Amani Botanical Garden at Muheza, Tanga region in 1971, 1977 and 1989.

Write and work in many publications of books within Tanzania and Globally.

Overview - Ethnobotany



Overview
Ethnobotany is considered a branch of ethnobiology, the study of past and present interrelationships between human cultures and the plants, animals, and other organisms in their environment. Like its parent field, ethnobotany makes apparent the connection between human cultural practices and the sub-disciplines of biology.
Historic roots of ethnobotany
Although ethnobotany did not emerge as an academic discipline until the end of the nineteenth century, its roots extend back to Greek, Roman, and Islamic sources. In 77 C.E., the Greek surgeon Dioscorides published De Materia Medica, a catalog of about 600 plants found in the Mediterranean. This illustrated book of herbal (a book that describes the appearance, medicinal properties, and other characteristics of plants used in herbal medicine), which influenced scholars through the Middle Ages, contained information on how and when each plant was gathered, its use by the Greeks, and whether or not it was edible. (Dioscorides even provided recipes.) He also assessed the economic potential of these plants.
Modern ethnobotany
Beginning in the twentieth century, the field of ethnobotany experienced a shift from the raw compilation of data to a greater methodological and conceptual reorientation. Today, the practice of ethnobotany requires a variety of skills:
  • botanical training for the identification and preservation of plant specimens
  • anthropological training to understand the cultural concepts around the perception of plants
  • linguistic training to transcribe local terms and understand native morphology, syntax, and semantics.
Ethnobotanists engage in a broad array of research questions and practices, which do not lend themselves to easy categorization. However, the following headings attempt to describe some of the key areas of modern study.


Ref. http://www.newworldencyclopedia.org/entry/Ethnobotany

Monday, November 4, 2013

Kitini cha kuanzisha kitalu cha miche ya miti.



KUANZISHA VITALU VYA MICHE YA MITI

KUCHAGUA SEHEMU YA KUANZISHA BUSTANI
·         Sehemu iwe na muinuko wa kiasi (1-5%)
·         Sehemu isiwe na mafuriko wakati wa mvua
·         Sehemu iwe karibu na maji ya bomba, mto, mfereji au ziwa.
·         Sehemu iwe na barabara inayopitika wakati wote wa mwaka
·         Sehemu iwe karibu na mahali miti itakapopandwa.
·         Sehemu isiwe na udongo wa mfinyazi au wenye chumvi

KUHUDUMIA MBEGU KABLA YA KUZISIA (SEED PRETREATMENT)
Mbegu nyingi katika jamii ya mikundekunde (Leguminasaceae) zina ganda gumu ambalo linazuia maji na hewa kupenya. Hivyo zinahitaji kuhudumiwa kabla ya kuzisia. K.m. mbegu ya mgunga (Acacia tortilis); maji yanayochemka yamiminwe kwenye mbegu  na kukorogwa mara kwa mara mpaka maji yapoe. Mbegu ambazo zitakua hazikuvimba zitenganishwe na zile zilizovimba halafu zilowekwe tena. Ziko njia nyingi za kuzikwangua kwa kisu, kutumia chombo kiitwacho bunduki ya mbegu (seed gun), waya wa moto (hoto wire) n.k.
JINSI YA KUTENGENEZA KITALU  
Fremu yenye kimo cha sm 25 – 30 itengenezwe kwa mbao (matofali au mawe pia yanaweza  kutumika). Upande mmoja wa fremu  ulazwe kiasi cha sm 5 chini ya ardhi. Upana wa kitalu unaweza kuwa meta 1 na urefu meta kadhaa kutegemeana na kaisi cha mbegu utakachosia.
Kitalu kijazwe  kwa tabaka kama ifuatavyo:-
1.      Chini; kokoto – Sm 5
2.     Katikakati: Mchanganyiko wa udongo wa tabaka la udongo wa juu                                kutoka msituni ni na mchanga, katika uwiano kwa nusu kwa ujazo – Sm10.
3.  Juu: Mchanga laini ambao mboji na tope/vumbi vimeondolewa – Sm5.
Kitalu kisijazwe mpaka juu kabisa. Ama sivyo mchanga wa juu pamoja na mbegu vitamomonyoka wakati wa kumwagilia maji. Juu ya kitalu mchanga usawazishwe na kushindiliwa kwa ubao ulio bapa. Kitalu kijengewe kibanda ili kuwe na kivuli kwa mbegu zinazoota. Kibanda kinaweza kuwa cha majani au fito zenye kipenyo cha Sm2 yaliyoshonwa kwa kamba kiasi cha Sm 2 kutoka fito hadi fito. Kibanda kiwe kiasi cha Meta 2 juu ya kitalu kwa kukiegemeza kwenye nguzo zilizofungwa pamoja na fito. Pande zote za kitalu ziachwe wazi ili hewa ipite kwa urahisi.

KUSIA MBEGU NA JINSI ZINAVYOOTA
Mbegu zisambazwe juu  ya kitalu. Nafasi kiasi cha mara mbili ya unene wa mbegu moja iachwe kutenganisha mbegu moja hadi nyingine ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa ukungu. Mbegu zifunikwe na mchanga kwa kina kaisi cha mara mbili ya unene wa mbegu yenyewe.
Kitalu kimwagiliwe maji kila mara kwa kutumia chombo chenye matundu madogomadogo kwa uangalifu ili mchanga usije ukalowa kupita kiasi. Wakati wa majira ya mvua mbegu zifunikwe kwa majani makavu halafu kivuli kiondolewe ili kuzuia uharibifu unaoweza kusababishwa na matone yanayondokoka kutoka juu ya kibanda.
Mienendo ya kuota  inatofautiana kati ya aina ya mti mmoja na mwingine. Mbegu zingine huanza kuota baada ya juma moja na kumaliza baada ya majuma mawili k.m mkwaju. Mbegu  za miti mingine huota rejareja kwa miezi mingi k.m mtiki (Tectona grandis) na msizi (Maesopsis eminii).

KUTAYARISHA MCHANGANYIKO WA UDONGO NA KUJAZA VIRIBA
Mchanganyiko wa udongo unaofaa kukuzuia miche  katika viriba ni:
·         Samadi
·         Mchanga
·         Udongo mzuri ni ule unatoka katika tabaka la juu katika msitu mnene. Huu usipopatikana udongo wa kawaida wa tabaka la juu katika kichaka au mboji itokanayo na marejea inaweza kutumika.
Vitu vyote vitatu vinavyohusika vichekechwe kwanza ili kuondoa mabonge na mawe pamoja na takataka. Kasha vichanganywe katika uwiano wa 1:2:4 kwa ujazo . kama mchanganyiko umekauka , unyunyiziwe maji kidogo na kukorogwa sawasawa. Mchanganyiko yafaa uwe mwepesi lakini ushikamane kiasi cha kuzuia usitoke wakati wa kuinua viriba. Makopo, mifuko ya nailoni, majani ya mgomba au mianzi (hapa vinaitwa viriba) vinaweza vikawa na Sm 6 za kipenyo (ambayo ni sm 10 au inchi 4 za upana vikawa bapa) na urefu wa Sm 14 au nchi 51 /2. Viriba vinaweza kuwa na rangi nyeusi au nyeupe. Viriba vijazwe kwa hatua na udongo ushindiliwe katika kila hatua. Viriba vikijazwa kwa mara moja nafsi ya hewa inatokea ndani.

KUPANDIKIZA MICHE KWENYE VIRIBA
Wakati Miche michanga imeanza kuota majani ya kwanza ing’olewe kwenye kitalu ipandikizwe kwenye viriba kama ifuatavyo: Kishimo kirefu zaidi kuliko mizizi ya miche kitengenezwe kwa kijiti ili mizizi isije  ikapinda kuelekea juu. Pia kishimo kiwe na upana wa kutosha, vinginevyo mizizi ya pembeni itashika ukikongoni na kupinda juu wakati mche ukiingizwa. Wakati wa kupandikiza, miche ishikwe tu kwenye ghala zake za chakula (Cotyledons) na sio kwenye shina.
Mizizi michanga inaweza kukatwa kama ikibidi ibakie sm 4 za urefu. Kila mche upandikizwe katika kila kiriba kwa kina kirefu kidogo kuzidi ilivyokuwa kwenye kitalu na udongo ushindiliwe vyema kandokando ya mizizi. Viriba visimamishwe wima ndani ya fremu zilizotengenzwa kama zile za kitalu ili kuzuia visianguke au kuchomwa na jua kwenye upande wa ubavuni.
Wakati mwingine mbegu hupandwa moja kwa moja katika viriba. Mbegu zinazofaa kwa njia hii ni zile amazo ni kubwa na uotaji wake ni mkubwa (zaidi y 80%. Kwa mfano:
Mkarati (bridelia micrantha), Msenefu (Croton megalocarpus),  Mkwaju (Tamarindus indica) Mafura (trichilia emetic), Mkangazi (Kyaya anthotheca),  Muarobaini (Azadirachta indica) n.k
Mbegu moja au mbili ziwekwe katikati ya kiriba kilichojazwa udongo na kisha kifunikwe na udongo wa aina ileile iliyotumika kujazia kiriba kwa kina cha Sm1.

KUTUNZA MICHE KATIKA BUSTANI
Miche iwekwe chini ya kivuli kama cha kitalu cha mbegu. Kunyweshea kufanyike kwa chombo chenye matundu madogomadogo kila asubuhi na jioni kadiri muda wa kupanda shambani upaokaribia kivuli kiondolowe polepole aidha kwa kupunguza majani kwenye kibanda au kwa kuondoa kibanda kwa muda mrefu zaidi kila siku mpaka miche itakapoweza kustahimili jua la moja kwa moja. Upunguzaji wa unyweshaji, dhidi ya mahitaji ya miche vitumike ili “kukomaza” miche tayari kwa upande wa kupanda shambani. Viriba visogezwe mara kwa mara ili mizizi inayojitokeza chini kwa kutumia kisu kikali. Viriba vinaweza kupaliliwa kwa kutumia kijiti chenye ncha kali au kutumia mkono. Wadudu waharibifu wanaweza kuzuiliwa kwa kunyunyiziwa dawa ya Dadmac (1% malathion) au Basudin 600C. kipimo cha kawaida cha miche inayofaa kwa kupanda shambani ni kiasi cha sm25-30. Miche hiyo huchukua miezi 4-10 kuikuza tangu siku ya kuipandikiza kutengemeana na mti inayohusika.

UPANDAJI NA UTUNZAJI WA MITI NA MATUMIZI MBALIMBALI
a)      Kutayarisha shamba
Inapendekezwa kuwa pale inapowezekana shamba lilimwe kabisa kabla ya kupanda. Gharama ya kulima inaweza ikapunguzwa kwa kuchanganya miti na mazao ya kilimo, yaani kilimo mseto (Agroforestry) kama vile pamba, mahindi, mtama, tumbaku n.k  Utaratibu huu pia unapunguza gharama ya kupalilia.
Miti mingine kama vile migriveria, mijohoro, miarobaini na mikenge inaweza kupandwa moja kwa moja katika mbuga mradi eneo kuzunguka shimo la kupandia mche limelimwa kabla ya kupanda.
b)     Majira ya kupanda
Kupanda miti kufanyike wakati wa mvua, yaani, wakati udongo una unyevuunyevu wa kutosha. Katika sehemu zenye mvua nyingi, ni rahisi kutekeleza jambo hili kwa sababu hali hiyo inaendelea kwa muda mrefu baada ya kuanza mvua za masika, wakati huo ni Machi na Aprili. Katika maeneo hayo inashauriwa kufuata majira yaleyale ya kupanda mazao ya chakula. Ni vizuri zaidi kupanda mara tu mvua za masika zinapoanza kunyesha.
KUTAYARISHA MASHIMO NA KUPANDA
Umbali kati  mti na mti hutegemea aina ya mti na madhumuni ya kuipanda. Iwapo madhumuni ni kuanzaisha shamba la miti (msitu) kwa kawaida umabli unaofaa ni mita 2.5 x 2.5 ambalo ni sawasawa na miti 1,600 kwa hekta 1. Kwa miti ambayo haikupandwa katika shamba la miti katika mtindo wa kilimo mseto, miti ipandwe kwa nafasi kufuatana na aina ya miti na matumizi, mfano: nguzo, malisho na uzio.
  
Mashimo yenye upana wa Sm 30 (ft 1) na kina Sm 30 yachimbwe kwa mstari kwa kutumia kamba kisha miche isafirishwe kwa unagalifu kutoka katika bustani na kupandwa katika shimo mara moja, Kiriba lazima kiondolewe kabla ya kupanda. Wakati wa kupanda ni vyema kufukia mche kwa kutumia udongo kuzunguka mche ushindiliwe kwa uangalifu bila kukata mizizi ya mche.
KUTUNZA SHAMBA LA MITI
a)      Kupalilia
Miti ya aina karibu zote haiwezi kuvumilia magugu. Isipopaliliwa mapema hudhoofika na hata kama baadaye ikipaliliwa itachukua muda mrefu kurudia hali yake ya awali. Miti mingine hufa kwa sababu ya magugu. Njia nzuri ya kuthibiti magugu ni kulima shamba vizuri kabla ya kupanda. Pale ambapo hakuna mazao ya kilimo, ni vyema kupalilia eneo lenye kipenyo cha m1 kuzunguka mti na pia kufyeka majani marefu kati ya miti.

b)     Kukatia matawi na kupunguza miti
Kwa baadhi ya miti ni vyema kukatia matawi ya chini katika kipindi cha miaka miwili ya mwanzo. Hii inasaidia wafanyakazi kupitia kwa urahisi katika shamba. Pia inazuia moto usisambae iwapo utatokea. Miti ya mbao kama vile msindano (Pine) na msanduku (Cypress) ina utaratibu maalumu uliowekwa (Pruning Schedule) wa kukatia matawi kulingana na umri na mahali ulipopandwa.
Aina nyingi za miti hazina utaraibu maalumu wa kuipunguza, lakini kila mti uliokufa sharti uondolewe ili kutoa nafasi ya miti iliyo na afya. Pia miti ya msindano na msanduku ina utaratibu maalumu wa kupunguza miti (Thinning schedule). Zoezi hili hutegemeana na matumizi yaliyokusudiwa k.m kuni, mbao na karatasi n.k








Misitu ni Uhai
Tuitunze Itutunze