KUANZISHA VITALU VYA MICHE YA MITI
KUCHAGUA SEHEMU YA KUANZISHA
BUSTANI
·
Sehemu iwe na muinuko wa kiasi (1-5%)
·
Sehemu isiwe na mafuriko wakati wa mvua
·
Sehemu iwe karibu na maji ya bomba, mto, mfereji au ziwa.
·
Sehemu iwe na barabara inayopitika wakati wote wa mwaka
·
Sehemu iwe karibu na mahali miti itakapopandwa.
·
Sehemu isiwe na udongo wa mfinyazi au wenye chumvi
KUHUDUMIA MBEGU KABLA YA KUZISIA
(SEED PRETREATMENT)
Mbegu
nyingi katika jamii ya mikundekunde (Leguminasaceae) zina ganda gumu ambalo linazuia
maji na hewa kupenya. Hivyo zinahitaji kuhudumiwa kabla ya kuzisia. K.m. mbegu
ya mgunga (Acacia tortilis); maji yanayochemka yamiminwe kwenye mbegu na kukorogwa mara kwa mara mpaka maji yapoe.
Mbegu ambazo zitakua hazikuvimba zitenganishwe na zile zilizovimba halafu
zilowekwe tena. Ziko njia nyingi za kuzikwangua kwa kisu, kutumia chombo
kiitwacho bunduki ya mbegu (seed gun), waya wa moto (hoto wire) n.k.
JINSI YA KUTENGENEZA KITALU
Fremu
yenye kimo cha sm 25 – 30 itengenezwe kwa mbao (matofali au mawe pia yanaweza kutumika). Upande mmoja wa fremu ulazwe kiasi cha sm 5 chini ya ardhi. Upana
wa kitalu unaweza kuwa meta 1 na urefu meta kadhaa kutegemeana na kaisi cha mbegu
utakachosia.
Kitalu kijazwe kwa tabaka kama ifuatavyo:-
1.
Chini; kokoto – Sm 5
2.
Katikakati: Mchanganyiko wa udongo wa tabaka
la udongo wa juu kutoka msituni ni na mchanga, katika
uwiano kwa nusu kwa ujazo – Sm10.
3.
Juu: Mchanga laini ambao mboji na
tope/vumbi vimeondolewa – Sm5.
Kitalu kisijazwe mpaka juu kabisa.
Ama sivyo mchanga wa juu pamoja na mbegu vitamomonyoka wakati wa kumwagilia
maji. Juu ya kitalu mchanga usawazishwe na kushindiliwa kwa ubao ulio bapa. Kitalu
kijengewe kibanda ili kuwe na kivuli kwa mbegu zinazoota. Kibanda kinaweza kuwa
cha majani au fito zenye kipenyo cha Sm2 yaliyoshonwa kwa kamba kiasi cha Sm 2
kutoka fito hadi fito. Kibanda kiwe kiasi cha Meta 2 juu ya kitalu kwa
kukiegemeza kwenye nguzo zilizofungwa pamoja na fito. Pande zote za kitalu
ziachwe wazi ili hewa ipite kwa urahisi.
KUSIA MBEGU NA JINSI ZINAVYOOTA
Mbegu zisambazwe juu ya kitalu. Nafasi kiasi cha mara mbili ya
unene wa mbegu moja iachwe kutenganisha mbegu moja hadi nyingine ili kuzuia
kusambaa kwa ugonjwa wa ukungu. Mbegu zifunikwe na mchanga kwa kina kaisi cha
mara mbili ya unene wa mbegu yenyewe.
Kitalu
kimwagiliwe maji kila mara kwa kutumia chombo chenye matundu madogomadogo kwa
uangalifu ili mchanga usije ukalowa kupita kiasi. Wakati wa majira ya mvua
mbegu zifunikwe kwa majani makavu halafu kivuli kiondolewe ili kuzuia uharibifu
unaoweza kusababishwa na matone yanayondokoka kutoka juu ya kibanda.
Mienendo ya kuota inatofautiana kati ya aina ya mti mmoja na
mwingine. Mbegu zingine huanza kuota baada ya juma moja na kumaliza baada ya
majuma mawili k.m mkwaju. Mbegu za miti
mingine huota rejareja kwa miezi mingi k.m mtiki (Tectona grandis) na msizi
(Maesopsis eminii).
KUTAYARISHA MCHANGANYIKO WA UDONGO NA KUJAZA VIRIBA
Mchanganyiko
wa udongo unaofaa kukuzuia miche katika
viriba ni:
·
Samadi
·
Mchanga
·
Udongo mzuri ni ule unatoka katika tabaka la juu katika
msitu mnene. Huu usipopatikana udongo wa kawaida wa tabaka la juu katika
kichaka au mboji itokanayo na marejea inaweza kutumika.
Vitu vyote vitatu vinavyohusika
vichekechwe kwanza ili kuondoa mabonge na mawe pamoja na takataka. Kasha
vichanganywe katika uwiano wa 1:2:4 kwa ujazo . kama mchanganyiko umekauka ,
unyunyiziwe maji kidogo na kukorogwa sawasawa. Mchanganyiko yafaa uwe mwepesi
lakini ushikamane kiasi cha kuzuia usitoke wakati wa kuinua viriba. Makopo,
mifuko ya nailoni, majani ya mgomba au mianzi (hapa vinaitwa viriba) vinaweza
vikawa na Sm 6 za kipenyo (ambayo ni sm 10 au inchi 4 za upana vikawa bapa) na
urefu wa Sm 14 au nchi 51 /2. Viriba vinaweza kuwa na rangi nyeusi
au nyeupe. Viriba vijazwe kwa hatua na udongo ushindiliwe katika kila hatua.
Viriba vikijazwa kwa mara moja nafsi ya hewa inatokea ndani.
KUPANDIKIZA MICHE KWENYE VIRIBA
Wakati Miche michanga imeanza kuota
majani ya kwanza ing’olewe kwenye kitalu ipandikizwe kwenye viriba kama
ifuatavyo: Kishimo kirefu zaidi kuliko mizizi ya miche kitengenezwe kwa kijiti
ili mizizi isije ikapinda kuelekea juu.
Pia kishimo kiwe na upana wa kutosha, vinginevyo mizizi ya pembeni itashika
ukikongoni na kupinda juu wakati mche ukiingizwa. Wakati wa kupandikiza, miche
ishikwe tu kwenye ghala zake za chakula (Cotyledons) na sio kwenye shina.
Mizizi michanga inaweza kukatwa
kama ikibidi ibakie sm 4 za urefu. Kila mche upandikizwe katika kila kiriba kwa
kina kirefu kidogo kuzidi ilivyokuwa kwenye kitalu na udongo ushindiliwe vyema
kandokando ya mizizi. Viriba visimamishwe wima ndani ya fremu zilizotengenzwa
kama zile za kitalu ili kuzuia visianguke au kuchomwa na jua kwenye upande wa
ubavuni.
Wakati mwingine mbegu hupandwa moja
kwa moja katika viriba. Mbegu zinazofaa kwa njia hii ni zile amazo ni kubwa na
uotaji wake ni mkubwa (zaidi y 80%. Kwa mfano:
Mkarati (bridelia micrantha), Msenefu (Croton megalocarpus), Mkwaju (Tamarindus indica) Mafura (trichilia
emetic), Mkangazi (Kyaya anthotheca), Muarobaini
(Azadirachta indica) n.k
Mbegu moja au mbili ziwekwe
katikati ya kiriba kilichojazwa udongo na kisha kifunikwe na udongo wa aina
ileile iliyotumika kujazia kiriba kwa kina cha Sm1.
KUTUNZA MICHE KATIKA BUSTANI
Miche
iwekwe chini ya kivuli kama cha kitalu cha mbegu. Kunyweshea kufanyike kwa
chombo chenye matundu madogomadogo kila asubuhi na jioni kadiri muda wa kupanda
shambani upaokaribia kivuli kiondolowe polepole aidha kwa kupunguza majani
kwenye kibanda au kwa kuondoa kibanda kwa muda mrefu zaidi kila siku mpaka
miche itakapoweza kustahimili jua la moja kwa moja. Upunguzaji wa unyweshaji,
dhidi ya mahitaji ya miche vitumike ili “kukomaza” miche tayari kwa upande wa
kupanda shambani. Viriba visogezwe mara kwa mara ili mizizi inayojitokeza chini
kwa kutumia kisu kikali. Viriba vinaweza kupaliliwa kwa kutumia kijiti chenye
ncha kali au kutumia mkono. Wadudu waharibifu wanaweza kuzuiliwa kwa
kunyunyiziwa dawa ya Dadmac (1% malathion) au Basudin 600C. kipimo cha kawaida
cha miche inayofaa kwa kupanda shambani ni kiasi cha sm25-30. Miche hiyo
huchukua miezi 4-10 kuikuza tangu siku ya kuipandikiza kutengemeana na mti
inayohusika.
UPANDAJI NA UTUNZAJI WA MITI NA
MATUMIZI MBALIMBALI
a)
Kutayarisha shamba
Inapendekezwa
kuwa pale inapowezekana shamba lilimwe kabisa kabla ya kupanda. Gharama ya
kulima inaweza ikapunguzwa kwa kuchanganya miti na mazao ya kilimo, yaani
kilimo mseto (Agroforestry) kama vile pamba, mahindi, mtama, tumbaku n.k Utaratibu huu pia unapunguza gharama ya
kupalilia.
Miti mingine kama vile migriveria,
mijohoro, miarobaini na mikenge inaweza kupandwa moja kwa moja katika mbuga mradi
eneo kuzunguka shimo la kupandia mche limelimwa kabla ya kupanda.
b)
Majira ya kupanda
Kupanda miti kufanyike wakati wa
mvua, yaani, wakati udongo una unyevuunyevu wa kutosha. Katika sehemu zenye
mvua nyingi, ni rahisi kutekeleza jambo hili kwa sababu hali hiyo inaendelea
kwa muda mrefu baada ya kuanza mvua za masika, wakati huo ni Machi na Aprili.
Katika maeneo hayo inashauriwa kufuata majira yaleyale ya kupanda mazao ya
chakula. Ni vizuri zaidi kupanda mara tu mvua za masika zinapoanza kunyesha.
KUTAYARISHA MASHIMO NA KUPANDA
Umbali
kati mti na mti hutegemea aina ya mti na
madhumuni ya kuipanda. Iwapo madhumuni ni kuanzaisha shamba la miti (msitu) kwa
kawaida umabli unaofaa ni mita 2.5 x 2.5 ambalo ni sawasawa na miti 1,600 kwa
hekta 1. Kwa miti ambayo haikupandwa katika shamba la miti katika mtindo wa
kilimo mseto, miti ipandwe kwa nafasi kufuatana na aina ya miti na matumizi,
mfano: nguzo, malisho na uzio.

Mashimo yenye upana wa Sm 30 (ft 1)
na kina Sm 30 yachimbwe kwa mstari kwa kutumia kamba kisha miche isafirishwe
kwa unagalifu kutoka katika bustani na kupandwa katika shimo mara moja, Kiriba
lazima kiondolewe kabla ya kupanda. Wakati wa kupanda ni vyema kufukia mche kwa
kutumia udongo kuzunguka mche ushindiliwe kwa uangalifu bila kukata mizizi ya
mche.
KUTUNZA SHAMBA LA MITI
a)
Kupalilia
Miti ya aina karibu zote haiwezi
kuvumilia magugu. Isipopaliliwa mapema hudhoofika na hata kama baadaye
ikipaliliwa itachukua muda mrefu kurudia hali yake ya awali. Miti mingine hufa
kwa sababu ya magugu. Njia nzuri ya kuthibiti magugu ni kulima shamba vizuri
kabla ya kupanda. Pale ambapo hakuna mazao ya kilimo, ni vyema kupalilia eneo lenye
kipenyo cha m1 kuzunguka mti na pia kufyeka majani marefu kati ya miti.
b)
Kukatia matawi na kupunguza miti
Kwa baadhi ya miti ni vyema kukatia
matawi ya chini katika kipindi cha miaka miwili ya mwanzo. Hii inasaidia
wafanyakazi kupitia kwa urahisi katika shamba. Pia inazuia moto usisambae iwapo
utatokea. Miti ya mbao kama vile msindano (Pine) na msanduku (Cypress) ina
utaratibu maalumu uliowekwa (Pruning Schedule) wa kukatia matawi kulingana na
umri na mahali ulipopandwa.
Aina nyingi za miti hazina utaraibu maalumu wa kuipunguza,
lakini kila mti uliokufa sharti uondolewe ili kutoa nafasi ya miti iliyo na
afya. Pia miti ya msindano na msanduku ina utaratibu maalumu wa kupunguza miti
(Thinning schedule). Zoezi hili hutegemeana na matumizi yaliyokusudiwa k.m
kuni, mbao na karatasi n.k
Misitu ni Uhai
Tuitunze Itutunze
No comments:
Post a Comment